mtoto.news

Vilabu vya shule vinasaidia katika kukuza talanta ya watoto.

August 22, 2022

Katika nchi ya Kenya, kutoka shule ya msingi na upili shughuli za ziada za masomo hufanyiwa katika vilabu vya shule.

Shughuli hizi mara nyingi huwa ni za kuwawezesha wanafunzi kujaribu kufanya vitu tofauti na masomo. Mifano ya shughuli hizi ni kama kucheza mpira, kushona nguo, kuchora, kucheza vifaa za muziki na kadhalika.

Aidha, vilabu hizi pia huwa na manufaa kwa watoto kwa sababu husaidia kukuza talanta zao. Mara nyingi, watoto hawa huweza kujua kile wanataka kufanya wakikuwa wakubwa.

Pia watoto hawa huweza kuingiliana na kujuana na watoto wengine, ambao sio wa darasa lao kisha kuwa marafiki. Marafiki hawa husaidia pia katika kukuza talanta kwa kuhimizana.

Mwaka jana, katibu wa baraza la mawaziri wa kilimo Anne Nyaga aliweza kuongelelea kuhusu kufufua kwa vilabu vya Young Farmers Club na 4k katika shule ya msingi na upili.

Hata hivyo, aliongeza kuwa sababu kuu ya kuanguka kwa klabu hizi ni kuwa wanafunzi huonyeshwa mitazamo hasi kuhusu kufanya kilimo na wale ambao huwa wameanguka mitihani.

Uzinduzi wa programu ya kilabu cha 4k katika shule ya msingi inaweza kuwatia moyo watoto na kuweza kubadilisha fikiria zao ili kujiunga na biashara ya kilimo.

Pia vilabu vingine kama vya dini, huweza kusaidia watoto kukuwa na mielekeo nzuri. Hii ni kwa sababu mara nyingi huku watoto huonyeshwa umuhimu wa kupenda wenzao bila ubaguzi. Vilabu kama hizi pia huweza kuonyesha watoto wengine talanta zao. Mfano kuhubiri.

 

 

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *