mtoto.news

Wanafunzi wasaidiwe na wazazi kuchagua shule za upili za daraja ya chini

August 22, 2022

Huku wanafunzi wa gradi la sita wakichagua shule za upili za daraja la pili, ambayo ilianza tarehe 15 hadi tarehe 30, Agosti.

Wanafunzi hawa wanafaa kupewa mawaidha maalum wanapofanya uchaguzi huu. Hii ni kwa sababu wanafunzi hawa bado ni wachanga na ni vyema walimu, walezi na wazazi kuingilia kati na kuweza kuwasaidia katika uchaguzi huu.

Kulingana na waziri wa elimu George Magoha, Januari 2023 wanafunzi milioni 2.51 ndio watakaojiunga na shule ya sekondari. Miongoni mwao wanafunzi milioni 1.27 watakuwa wa gradi la sita.

Hii inaonyesha kuwa wanafunzi hawa watakuwa wengi mno. Licha ya hayo, mwaka zilizopita tumeshuhudia wanafunzi wa darasa la nane wakichagua shule zilizo mbali na kwao. Hii imewafanya wazazi kuteseka kuwatafutia shule zingine tena.

Pia wanafunzi hawa wamekuwa wakichagua shule za kifahari na hii imewafanya kukosa nafasi katika shule ambazo wangefaa kuenda.
Kwa hivyo, inafaa kuangaliwa kuwa wanafunzi wa gradi la sita ni wachanga. Wanafaa waongozwe kikamilifu na wakubwa wao Ili waweze kuchagua shule zilizo karibu na mahali wanapoishi. Hii itachangia katika kukuza usalama wa wanafunzi wanapojiunga na shule za upili.

Wizara ya elimu pia inafaa kuzingatia kuwa wanafunzi hawajaitwa shule zilizo mbali. Hii ni kwa sababu pia miaka zilizopita, kumekuwa na malalamishi kuwa serikali imekuwa ikiwaita wanafunzi shule za mbali, licha ya wanafunzi kuchagua shule walizopendelea.

Aidha, wanafunzi wanafaa pia kuonyeshwa mwelekeo wa kile wanachohitajika kufanya kabla na baada ya kujiunga na shule ya upili. Hii ni kwa sababu, watakuwa wa kwanza nchini kuanza mfumo huu mpya wa CBC.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *