mtoto.news

Shule Kadhaa Kusalia Kufungwa Jumatatu

August 23, 2022

Waziri wa Elimu George Magoha anasema kuwa, shule zilizo katika maeneo manane ya uchaguzi ambapo uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Jumatatu zitasalia kufungwa kwa siku moja.

Magoha alisema kwamba, uamuzi huo umechukuliwa ili kufungua njia kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutumia vituo hivyo kama vituo vya kupigia kura.

“Watoto wanaweza kukaa nyumbani Jumatatu 29, na kuripoti shuleni Jumanne tarehe 30. Kwa zile shule zenye mchanganyiko ambazo ni za Bweni na za mchana, wasomi wa Bweni wanapaswa kubaki shuleni na kuwa mbali na maeneo ya kupigia kura,” alisema.

Waziri wa Elimu hata hivyo aliitaka IEBC kuhamishia vituo vya kujumlisha kura katika vyuo vya elimu ya juu katika mikoa ili wanafunzi wanaofanya mitihani yao ya kitaifa mwaka huu wasikatishwe masomo yao.

CS Magoha pia aliwahakikishia wazazi kuwa watoto wao watakuwa salama katika kipindi hicho.

Tume ya IEBC inatazamiwa kufanya uchaguzi wa ugavana katika kaunti za Kakamega na Mombasa.

Kura za wabunge zitafanyika Rongai, Kitui Vijijini, Pokot Kusini na Kacheliba.

Wakaazi wa eneo la Nyaki Magharibi kaunti ya Meru na wadi ya Wanjenga kaunti ya Kiambu pia watapiga kura kuchagua Wabunge wa Bunge la Kaunti hiyo.

Hey, like this? Why not share it with a buddy?

One reply on “Shule Kadhaa Kusalia Kufungwa Jumatatu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *