Wazazi wengi wameonyesha hasira yao mitandaoni baada ya picha ya wanafunzi wakitoa kuku manyoya kusambaa mitandaoni.
Wananchi walionyesha wasiwasi kupitia twitter, huku wakikashifu mtaala wa CBC na wakisema kwamba, usalama wa watoto hao haukuzingatiwa kamwe, kwani kulikuwa na utumiaji wa visu na maji ya moto wakati wa matayarisho hayo ya kuku.
I don't like CBC and I am disappointed in the child endangerment present here. There was hot water involved and knives. How was one teacher supervising all that? Is this exercise in the syllabus or just in wherever Didmus comes from?
— Karrymi C. (@karrymi) September 17, 2022
Wengine wanadai kwamba, huu ni uwizi hadharani kwani shule zingine zinaitisha senti kutoka kwa watoto kwa madai ya minajili ya mafunzo ya uanzisho wa pesa kihistoria.
This is misuse of cbc. Like the other school in JUJA I heard that they are being taught about money they started with each student coming with 10, 20, 50 and then 100/- say you have 500 student is this not thuggery since the cash is left at school
— Francis Mbugua (@mbuguawairimu) September 18, 2022
Mwalimu Dida pia ameeleza kusikitishwa kwake na mfumo wa CBC akidai kwamba, haujafikia matarajio aliyokuwa nayo hapo awali.
When CBC was introduced, I was very excited. I naively thought it would teach pupils computer programming and other globally competitive courses to bring them to standards of China and South Korea. I never thought they would be asked to wear feathers like hawks and roast chicken!
— Mwalimu Dida Kipkoech Kinuthia (@mwalimu_dida) September 17, 2022
Kila jambo lililo na ubaya, pia lina uzuri wake, hata baada ya wanamitandao wengi kukashifu mfumo wa CBC bado kuna wengi ambao wanauunga mkono.
Wizara ya Elimu imekimbilia kutetea Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC)baada ya kuwepo na hofu ya uwezekano wa mtaala huo kufanyiwa marekebisho au kufutiliwa mbali kabisa na serikali mpya.
Kupitia taarifa ya kwanza ya utekelezaji ya CBC-Volume 1, Katibu wa Baraza la Mawaziri la Elimu Prof George Magoha anasema kuwa mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulioanzishwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ulikuwa umepita manufaa yake.
“Mazingira ya sasa ni tofauti sana na mfumo wa elimu wa 8-4-4. Sasa tuko katika jamii inayotegemea maarifa inayokabiliwa na changamoto, vikwazo na fursa zinazobadilika kila mara. Hii inahitaji aina mpya ya elimu…elimu ambayo inawapa wanafunzi sio ujuzi tu, bali pia uwezo wa kujifunza, ” Magoha anasema.
Hata hivyo, Mwanamtandao alitoa maoni na kusema kwamba, wanafunzi ndio wanafaa kupewa kipaumbele kwani mfumo huu umewekwa kwa ajili ya manufaa na mwanafunzi na wala sio kwa lingine lile.
This CBC issue, the goverment should interview the learners. If they are enjoying it, the parents should just step up.
CBC is meant for the benefit of the learners not the convinience of the parents.Miguna Miguna Madvd Whatsapp Jose carmago Ruto Gachagua
— VESSEL OF HONOR (@AnointedVOH) September 19, 2022
Aidha, shule nyingi za kibinafsi zimetoa maridhio yao ya kuchagua Mtaala wa Kimataifa iwapo CBC itafutiliwa mbali.
Leave a Reply