Rais William Ruto amesisitiza dhamira ya serikali ya Kenya Kwanza katika kutokomeza ukeketaji hadi mwisho wa kipindi chake.
Akizungumza siku ya Jumatatu, Ruto amesema kwamba, kesi za ukeketaji katika kipindi chake zitaondolewa.
“Ninakubaliana na CJ Martha Koome kwamba hatufai kuwa na mazungumzo kuhusu ukeketaji nchini Kenya katika Karne ya 21,” alisema. “Ninataka kuwahakikishia uungwaji mkono kutoka kwa utawala wangu katika kutokomeza ukeketaji kwani ni jambo la kurudi nyuma na inahatarisha afya ya wasichana wetu,” Ruto aliongeza.
Jaji Mkuu Martha Koome amekuwa mstari wa mbele katika kusukumana na vita dhidi ya ukeketaji. Koome ametoa wito kwa Wakenya ili kuzidisha vita dhidi ya ukeketaji na ndoa za utotoni. Martha amesema kuwa, sera na sheria za serikali zinapaswa kuwa na lenzi ya jinsia kuhusiana na takwimu zinazotumika, uchambuzi wa matrix ya kijinsia na ushiriki wa wanawake na wasichana katika utungaji wa sera.
Mnamo 2019, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta alijitolea kukomesha tabia hiyo ya ukeketaji nchini Kenya ifikapo Desemba 2022. Wakati huo huo, Sheria ya Marufuku ya FGM, ya 2011 ilianzisha bodi ya Kupinga FGM iliyopewa jukumu la kubuni, kusimamia, na kuratibu programu za uhamasishaji wa umma dhidi ya mila ya ukeketaji miongoni mwa majukumu mengine.
Leave a Reply