Mabadiliko ya hali ya hewa bado yanaendelea kuwa mwiba mchungu katika maeneo tofauti tofauti ya Kenya. Taita Taveta ni miongoni mwa Kaunti ambazo zinakubwa na athari hizi za mabadiliko ya hali ya hewa.
Ukosefu wa maji na chakula kutokana na kukauka kwa vyanzo vya maji katika Kaunti hiyo, kumewalazimisha wakaazi wa eneo hilo kusafiri kwa masaa marefu na kupanga foleni ili waweze kupata maji. Isitoshe hadi sasa ni kaya asilimia 52 tu ambazo zinaweza kumudu chakula chenye afya.
Asilimia 23 ya watoto wa Kaunti hiyo haswa kutoka maeneo ya kishushe wako kwenye hatari ya kupata mtapiamlo mkali, huku kuna hofu kwamba, tayari takriban watoto elfu tatu wameambukizwa na ugonjwa huo. Kulingana na taasisi za afya katika Kaunti hiyo, kumesemakana kwamba kwa kila wiki, visa kumi vya watoto walio na utapiamlo vinaripotiwa, huku kwa kila mwezi, visa mia mbili vinaripotiwa kutoka hospitali zote za maeneo hayo.
Aidha visa hivyo vinaendelea kuongezeka siku baada ya siku.
Zaidi ya hayo, Elimu na usalama wa watoto na wakaazi wa Kaunti ya Taita Taveta uko hatarini, kwani wanyama pori kama vile ndovu wameweza kuingia kwenye nafasi zao za kuishi na shule kwenye maeneo hayo. Madumu ya maji yanaonekana yakiwa yamevunjwa na ndovu wanapotafuta maji ya kunywa, jambo ambalo limefanya maisha ya wakaazi hao yawe magumu mno, huku ikiwalazimu watoto kuwacha shule.
Leave a Reply