Wakati migogoro inapotokea, basi watoto ndio waumiao zaidi.
Jumatatu tarehe 20 2023 wiki iliyopita, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, aliitisha Maandamano ya nchi nzima ili kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya na ushindi wa rais William Ruto katika uchaguzi.
Ikifwatia habari inayosema kwamba mwanafunzi wa chuo kikuu aliuawa huku zaidi ya watu 200 kukamatwa katika maandamano hayo, hofu kuu inaangukia maandamano haya kwani mwisho wa siku maandamano haya huleta vurugu, majeraha na hata vifo.
Isitoshe, kiongozi mpinzani Bwana Odinga, alinena kwamba maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika kila jumatatu kwa wiki kadhaa. Huu ni wakati nyeti mno kwa kila mwananchi, kwani watoto wengi walishindwa kwenda shuleni huku wengine wao wakishiriki maandamano hayo pamoja na wazazi wao au walezi wao.
Wananchi wengi wameonyesha wasiwasi wao mitandaoni baada ya picha inayooshesha mzazi na mtoto wake kwenye maandamano ya leo kusambaa mitandaoni.
Children should not be engaged in #Demonstrations, this is dangerous #MaandamanoMondays #Maandamano pic.twitter.com/9JdN7fca0T
— Almamy Moha (@AlmamyMoha_) March 27, 2023
Aidha wazazi wengine wameonyesha hofu yao juu ya watoto wao wanaoenda shuleni leo hii, kwa kuwaonya polisi kupitia mtandao wa twitter kwamba, wasirushe vitoa machozi na mawe kwani hilo linaweza kuwadhuru watoto, huku wakisisitiza kwamba, kila mtoto ana haki ya ulinzi anapoenda shuleni.
1.Dear Kenya police.We the parents of Nairobi will be sending our children to various schools today and infered from how you just throw teargas and stones we believe you,ll do so to our children.Please don't because if you do we will join the Maandamano. #MaandamanoMondays
— Hassanbajun Happiest (@hassanbajuun) March 27, 2023
Hata hivyo, viongozi wa kidini, miungano na kisiasa wanawataka Mheshimiwa Ruto na Raila kuketi chini na kuanzisha mazungumzo ili kunusuru nchi dhidi ya machafuko. Viongozi hao walisema kwamba, kizazi kijacho kitawawajibisha iwapo misimamo yao mikali itateketeza nchi.
Leave a Reply