mtoto.news

Categories
Child Rights FGM Health

Ruto Aahidi Kutokomeza Ukeketaji

 

Rais William Ruto akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Mwaka ya Utawala wa Haki nchini Kenya 2021/22 Picha: Twitter NCAJ Kenya

Rais William Ruto amesisitiza dhamira ya serikali ya Kenya Kwanza katika kutokomeza ukeketaji hadi mwisho wa kipindi chake.


Akizungumza siku ya Jumatatu, Ruto amesema kwamba, kesi za ukeketaji katika kipindi chake zitaondolewa.

“Ninakubaliana na CJ Martha Koome kwamba hatufai kuwa na mazungumzo kuhusu ukeketaji nchini Kenya katika Karne ya 21,” alisema. “Ninataka kuwahakikishia  uungwaji mkono kutoka kwa utawala wangu katika kutokomeza ukeketaji kwani ni jambo la kurudi nyuma na inahatarisha afya ya wasichana wetu,” Ruto aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *