Naam, mara nyingi kila mtu huimba, “Elimu kwa wote”, “Elimu ya bure”, ila ukweli wa mambo ni kwamba, elimu iko na bei ya juu mno, jambo linalowafanya watoto wengi wakose kupata masomo. Ahadi ya elimu ya msingi na sekondari kwa wote ni mojawapo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu . Hata hivyo mwaka wa 2020, takriban watoto milioni 64 […]
Author: khadija Mbesa
Zaidi ya wanafunzi 4,000 kutoka eneo bunge la Isiolo Kaskazini watapokea Sh. milioni 25.5 kama ufadhili katika jitihada za kuhakikisha kwamba wanafunzi wanasalia shuleni licha ya ukame unaoshuhudiwa na gharama kubwa ya maisha nchini. Kulingana na Mbunge wa Isiolo Kaskazini Bw Joseph Samal ambaye amezindua Sh. Milioni 25.5 za ufadhili zitakazowanufaisha wanafunzi 4,326 kutoka jimboni […]
Kulingana na Utafiti wa Demografia na Afya wa Kenya wa 2022, asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 19 wamewahi kupata mimba. Takwimu hii huongezeka kila wanakuwa wakubwa kutoka asilimia 3 kati ya watoto wa miaka 15 hadi asilimia 31 kati ya wale wenye umri wa miaka 19. Hii […]
Katika azma yake ya kufikia mabadiliko ya asilimia 100 kutoka shule ya msingi hadi ya upili, Utawala wa Serikali ya Kitaifa na Wizara ya Elimu wanapanga kufanya msako wa nyumba hadi nyumba, ili kuwatafuta wanafunzi waliopotea ambao walifanya mtihani wao wa Cheti cha Elimu ya Sekondari nchini Kenya mwaka jana. Kundi la viongozi katika […]
Beatrice Mwende, mwalimu wa Hisabati anayeishi Naivasha ambaye aliwaua watoto wake wanne mnamo Juni 2020, atatumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji hayo. Jaji wa Mahakama Kuu ya Naivasha Grace Nzioka alipuuzilia mbali utetezi wa Mwende kwamba alikuwa na mapepo alipowaua binti zake watatu na mwanawe mmoja. Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka […]
Mawaziri na wawakilishi kutoka nchi 12 za Afrika wamejitolea na kuweka mipango ya kumaliza UKIMWI kwa watoto ifikapo mwaka 2030. Nchi hizo ziliahidi kwamba, zitahakikisha watoto wote wenye VVU wanapata matibabu ya kuokoa maisha na hata akina mama wanaoishi na ugonjwa huo hawataweza kuwasambazia watoto wao. Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano ulioandaliwa na Tanzania, washirika wa […]
Suala la changamoto za ulinzi wa watoto katika jamii na shule ni jambo la kusikitisha mno, kwani mara nyingi wanafunzi ndio waathiriwa, huku wahusika wakuu wakiwa walimu wao. Kati ya mwaka wa 2014 na 2019, takriban walimu 125 kwa mwaka waliachishwa kazi na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kwa sababu ya unyanyasaji wa kijinsia […]
Rais wa Kenya, William Ruto, aita wito wa Nchi zote Afrika, katika kuungana mkono ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mataifa maskini, hasa yaliyomo barani Afrika, yameathiriwa vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa, huku ikizidisha ukame na mafuriko. Rais William Ruto amesema kwamba, sasa ni wakati muafaka kwa Afrika kukabiliana na mabadiliko […]
Wazazi katika Kaunti ya Pokot Magharibi wameonywa dhidi ya kukwepa majukumu yao ya uzazi, na kuhimizwa kutanguliza elimu ili kukuza vizazi vya kesho. Kamishna Msaidizi wa Kaunti ya Tapach (ACC) Ibrahim Masiaga alibainisha kuwa, ofisi yake imekuwa ikishughulikia visa vingi vya utelekezaji wa watoto, haswa katika suala la watoto wale waliokusudiwa kuvuka kidato cha kwanza […]
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku vitabu kadhaa vya watoto vinavyoashiria elimu ya ngono, kwa madai ya kukiuka “mila na desturi za maadili” katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambapo ushoga ni uhalifu. “Tunapiga marufuku vitabu hivi katika shule na miundo mingine ya elimu kwa sababu ni kinyume na viwango vya kitamaduni na maadili,” Waziri […]