mtoto.news

Categories
Latest News

Kenya: Wasiwasi Juu ya Mmiminiko wa Watoto Walemavu Mijini

Dkt Marion Karimi ambaye anaendesha kituo cha uokoaji na ukarabati wa watoto walemavu alikashifu kuwa katika miaka ya hivi majuzi idadi ya watoto wenye matatizo ya kimwili imekuwa ikiongezeka. Karimi ambaye kwa sasa anakarabati watoto 177 walemavu waliookolewa kutoka sehemu tofauti za nchi alibainisha kuwa watoto hao huwa wanatumiwa vibaya na watu wasiojulikana ili kuomba […]

Categories
Child Rights Education Education education

Mashirika Ya Hifadhi Kutumia Sh78 Milioni Kwa Watoto Wanaoishi Katika Mazingira Magumu

Zaidi ya wanafunzi 12,000 wenye uhitaji kutoka kaunti za Marsabit, Isiolo, Samburu na Laikipia watanufaika na ufadhili kutoka kwa shirika la Northern Rangeland Trust (NRT) ili kufadhili elimu yao. Afisa mkuu mtendaji wa NRT Tom Lalampaa alisema kuwa, shirika hilo litatumia milioni Sh78.5 kwa wanafunzi 12,557 wanaohitaji. Bw Lalampaa alisema kuwa, wahafidhina 18 wametanguliza elimu […]

Categories
Child Rights FGM Uncategorized

Sera Ya Ulinzi Wa Watoto Katika Kaunti Ya Samburu Yaendelea

IDARA ya Huduma kwa Watoto katika Kaunti ya Samburu imeanza juhudi za kuunda Sera ya Ulinzi wa Mtoto ambayo inawiana na changamoto za kipekee zinazowakabili watoto. Akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto wa Samburu (CPN), Afisa wa Watoto wa Samburu Peter Mwangi alisema kuwa uundaji wa CPN unalenga kuwaleta […]

Categories
Child Rights Education Latest News

Watoto Wasishirikishwe Kwenye Maandamano

Wakati migogoro inapotokea, basi watoto ndio waumiao zaidi. Jumatatu tarehe 20 2023 wiki iliyopita, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, aliitisha Maandamano ya nchi nzima ili kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya na ushindi wa rais William Ruto katika uchaguzi. Ikifwatia habari inayosema kwamba mwanafunzi wa chuo kikuu aliuawa huku zaidi ya watu 200 […]

Categories
Child Rights Latest News

Kesi ya Wizi wa Watoto Dhidi ya Deya imesogezwa hadi Aprili

Mahakama ya Nairobi imeahirisha kesi ya wizi wa watoto dhidi ya Askofu Gilbert Juma Deya baada ya hakimu wa mahakama kusema  alikuwa mgonjwa. Deya, ambaye alifika mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Robison Ondieki hapo jana, alikuwa tayari kwa kusikilizwa na kujitetea pamoja na wakili wake John Swaka. Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Nicholas […]

Categories
Child Rights

Kifungo cha Maisha kwa Kosa la Kunajisi Mtoto Nchini Kenya

Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya inaonyesha kuwa msichana mmoja kati ya wanne na mvulana mmoja kati ya kila mvulana tisa hudhulumiwa kingono kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Ripoti hiyo pia inafichua kuwa ni asilimia 41 tu ya wanawake na asilimia 39.2 ya wanaume waliokumbana na aina yoyote ya ukatili ndio walioweza […]

Categories
Child Rights Latest News OCSEA

Beatrice Mwende; Aliyewaua Watoto Wake Wanne Ahukumiwa Kifungo cha Maisha

    Beatrice Mwende, mwalimu wa Hisabati anayeishi Naivasha ambaye aliwaua watoto wake wanne mnamo Juni 2020, atatumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji hayo. Jaji wa Mahakama Kuu ya Naivasha Grace Nzioka alipuuzilia mbali utetezi wa Mwende kwamba alikuwa na mapepo alipowaua binti zake watatu na mwanawe mmoja. Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka […]

Categories
Data Stories

Tujitahidi Kutengeneza Mazingira Salama Ambapo Watoto Wanaweza Kujifunza na Kukua

Suala la changamoto za ulinzi wa watoto katika jamii na shule ni jambo la kusikitisha mno, kwani mara nyingi wanafunzi ndio waathiriwa, huku wahusika wakuu wakiwa walimu wao. Kati ya mwaka wa 2014 na 2019, takriban walimu 125 kwa mwaka waliachishwa kazi na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kwa sababu ya unyanyasaji wa kijinsia […]

Categories
Child Rights Education Education education

Wazazi Waonywa Dhidi ya Kuwatelekeza Watoto Wao

Wazazi katika Kaunti ya Pokot Magharibi wameonywa dhidi ya kukwepa majukumu yao ya uzazi, na kuhimizwa kutanguliza elimu ili kukuza vizazi  vya kesho. Kamishna Msaidizi wa Kaunti ya Tapach (ACC) Ibrahim Masiaga alibainisha kuwa, ofisi yake imekuwa ikishughulikia visa vingi vya utelekezaji wa watoto, haswa katika suala la watoto wale waliokusudiwa kuvuka kidato cha kwanza […]

Categories
Education Education education

Elimu Bora kwa Wote

Serikali imedhamiria kushughulikia matatizo yanayokwamisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto hasa wale walio katika Maeneo Kame na Nusu Kame (ASALs) nchini. Katibu wa Baraza la Mawaziri la Elimu Bw. Ezekiel Machogu alisema serikali imeanzisha Baraza la Kitaifa la Elimu ya Wahamaji nchini Kenya (NACONEK) ili kutoa miundo na kusaidia elimu katika maeneo yote ya […]