Wadau na wazazi walio na watoto walioathiriwa na usonji wamejitokeza na kutoa wito kwa serikali ya kitaifa na kaunti kuweka vifaa vitakavyowahudumia na kusaidia katika maendeleo ya watoto hao. Akihutubia wanahabari huko Uriri wakati wa Siku ya Autism Duniani, Caroline Kisuge wa Jonathan Rays of Hope alisema kuwa nchi haina vifaa vya kujifunzia ambavyo vinaweza […]
Author: khadija Mbesa
IDARA ya Huduma kwa Watoto katika Kaunti ya Samburu imeanza juhudi za kuunda Sera ya Ulinzi wa Mtoto ambayo inawiana na changamoto za kipekee zinazowakabili watoto. Akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Mtandao wa Ulinzi wa Mtoto wa Samburu (CPN), Afisa wa Watoto wa Samburu Peter Mwangi alisema kuwa uundaji wa CPN unalenga kuwaleta […]
Wakati migogoro inapotokea, basi watoto ndio waumiao zaidi. Jumatatu tarehe 20 2023 wiki iliyopita, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, aliitisha Maandamano ya nchi nzima ili kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya na ushindi wa rais William Ruto katika uchaguzi. Ikifwatia habari inayosema kwamba mwanafunzi wa chuo kikuu aliuawa huku zaidi ya watu 200 […]
Mahakama ya Nairobi imeahirisha kesi ya wizi wa watoto dhidi ya Askofu Gilbert Juma Deya baada ya hakimu wa mahakama kusema alikuwa mgonjwa. Deya, ambaye alifika mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Robison Ondieki hapo jana, alikuwa tayari kwa kusikilizwa na kujitetea pamoja na wakili wake John Swaka. Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Nicholas […]
Maji ni uhai, vile vile maji ni jambo muhimu mno katika maisha ya binadamu, Usafi wa mazingira na usafi kwa ujumla huzuia ueneaji wa magonjwa na maambukizi mbali mbali. Na iwapo maji yatakosekana, basi mahitaji mengi ya kimsingi pia yatakosekana. Watoto wengi hufa kutokana na ugonjwa wa kuhara, elimu yao huvurugika au kukwama, na utapiamlo […]
Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto kwa bahati mbaya ni mwiko kwenye jamii zetu, na mara nyingi, hakuna anayejadili suala hili licha ya kuenea kwake katika jamii. Walakini, wakati tutakapojitahidi kuleta mwanga kwenye ukweli huu, basi tutaweza kuokoa watoto wengi mno. Tafadhali soma mambo haya kumi, yaliyo na ukweli kuhusu unyanyasaji wa kingono kwa watoto, na […]
Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya inaonyesha kuwa msichana mmoja kati ya wanne na mvulana mmoja kati ya kila mvulana tisa hudhulumiwa kingono kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Ripoti hiyo pia inafichua kuwa ni asilimia 41 tu ya wanawake na asilimia 39.2 ya wanaume waliokumbana na aina yoyote ya ukatili ndio walioweza […]
Naam, mara nyingi kila mtu huimba, “Elimu kwa wote”, “Elimu ya bure”, ila ukweli wa mambo ni kwamba, elimu iko na bei ya juu mno, jambo linalowafanya watoto wengi wakose kupata masomo. Ahadi ya elimu ya msingi na sekondari kwa wote ni mojawapo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu . Hata hivyo mwaka wa 2020, takriban watoto milioni 64 […]
Zaidi ya wanafunzi 4,000 kutoka eneo bunge la Isiolo Kaskazini watapokea Sh. milioni 25.5 kama ufadhili katika jitihada za kuhakikisha kwamba wanafunzi wanasalia shuleni licha ya ukame unaoshuhudiwa na gharama kubwa ya maisha nchini. Kulingana na Mbunge wa Isiolo Kaskazini Bw Joseph Samal ambaye amezindua Sh. Milioni 25.5 za ufadhili zitakazowanufaisha wanafunzi 4,326 kutoka jimboni […]
Kulingana na Utafiti wa Demografia na Afya wa Kenya wa 2022, asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 19 wamewahi kupata mimba. Takwimu hii huongezeka kila wanakuwa wakubwa kutoka asilimia 3 kati ya watoto wa miaka 15 hadi asilimia 31 kati ya wale wenye umri wa miaka 19. Hii […]