Wizara ya afya nchini humo imesema kwamba, idadi ya vifo vya watoto vilivyotokana na Ugonjwa huo vimeongezeka hadi karibia 700.

Wizara ya afya nchini humo imesema kwamba, idadi ya vifo vya watoto vilivyotokana na Ugonjwa huo vimeongezeka hadi karibia 700.
Zaidi ya watoto milioni tatu wanahitaji msaada wa kibinadamu na wako katika hatari kubwa ya magonjwa yanayotokana na maji, kuzama na utapiamlo kutokana na mafuriko makubwa zaidi katika historia ya hivi majuzi ya Pakistan
Ukame mkali katika kaunti ya Marsabit unatatiza masomo ya watoto, huku wengi wao wakilazimika kuacha shule.
Mtaalamu Mwandamizi wa Mpango wa Elimu katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),Saidou Sireh Jallow, aliliambia kongamano la elimu kuwa Kenya imeweka kipaumbele katika uwekezaji wa umma katika elimu, hii ikisababisha mwelekeo wa kupanda kwa viashiria vingi vya maendeleo ya elimu. . […]
Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Kiambu wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi wa kidato cha kwanza anadaiwa kuwaua ndugu zake watatu na binamu yake katika muda wa mwaka mmoja uliopita. Kulingana na KBC, Mtoto huyo alipokuwa katika kituo cha Polisi cha Kikuyu, alikiri kwa wapelelezi jinsi alivyowaua ndugu zake, mmoja akiwa na umri wa miezi 15, […]
Waziri wa Elimu George Magoha amefutilia mbali kuongezwa kwa kalenda ya shule baada ya shinikizo kutoka kwa wakuu wa shule wa sekta ya elimu. Akizungumza baada ya kufungua madarasa ya mtaala unaozingatia umahiri huko Njiru, Magoha alisema kuwa wizara ina nia ya kuhakikisha kalenda ya shule inarudi kuwa ya kawaida mnamo Januari. Alisema kuwa kufikia […]
Waziri wa Elimu George Magoha anasema kuwa, shule zilizo katika maeneo manane ya uchaguzi ambapo uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Jumatatu zitasalia kufungwa kwa siku moja. Magoha alisema kwamba, uamuzi huo umechukuliwa ili kufungua njia kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutumia vituo hivyo kama vituo vya kupigia kura. “Watoto wanaweza kukaa nyumbani Jumatatu […]
Takriban watoto bilioni moja walio na umri wa miaka 2-17 huathiriwa na ukatili wa kimwili, kingono, au kihisia kila mwaka.
mlipuko wa surua nchini Zimbabwe umewaua watoto 157, wengi wao wakiwa hawajachanjwa kutokana na imani za kidini za familia zao.
Kulingana na Save the Children wazazi kutoka kaskazini-mashariki mwa Uganda wanalazimika kuwatuma watoto wao wachanga wa umri wa shule ya awali, shuleni pamoja na ndugu zao ili waweze kushiriki kwenye mlo wa bure shuleni kwani idadi ya familia zisizoweza kumudu chakula nyumbani inazidi kuongezeka. Natalina, aliye na miaka 10, anasoma katika shule ya jumuiya inayoungwa […]