mtoto.news

Categories
Data Stories Health Uncategorized

Kenya: Watoto milioni 16 hatarini kutokana na umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa

Takriban watoto milioni 16.4 nchini Kenya, ambayo ni sawa na asilimia 67 ya idadi ya watoto nchini humo, wameathiriwa na umaskini na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

Categories
Uncategorized

Uganda: Maafa ya moto yaua zaidi ya watoto 10

Chanzo cha moto katika shule ya bweni huko Mukono, mashariki mwa mji mkuu, Kampala, kinachunguzwa huku watoto wanne wako katika hali mbaya na wanatibiwa hospitalini. Wazazi waliofadhaika wamekusanyika kwenye tovuti. Dkt Moses Keeya, anayefanya kazi katika hospitali ya eneo hilo iliyopokea majeruhi kwa mara ya kwanza, alisema “walipata majeraha mengi kwenye mikono, miguu na kifua. […]

Categories
Education Education education Uncategorized

Kilifi: Ukosefu wa madarasa, changamoto kwa utekelezaji wa CBC

Wakati kikundi kazi cha wanachama 49 kinajadili jinsi ya kurekebisha sekta ya elimu kwa mtaala unaozingatia umahiri kama kazi yake ya kwanza, walimu na wanafunzi katika maeneo ya mbali yaliyokumbwa na ukame wanatatizika kuendana na majukumu mapya kulingana na mtaala. Lakini kazi hizo ni kidokezo tu kwani ukosefu wa vyumba vya madarasa umefanya mchakato wa […]

Categories
Health Latest News

Dawa za sharubati zapigwa marufuku baada ya vifo vya watoto 99.

Vifo vya karibu watoto 100 nchini Indonesia vimesababisha nchi hiyo kusimamisha uuzaji wa dawa zote za sharubati. Ni wiki chache tu baada ya dawa ya kikohozi nchini Gambia kuhusishwa na vifo vya karibia watoto 70. Indonesia imesema kwamba, baadhi ya dawa za sharubati zimepatikana kuwa na viambato vinavyohusishwa na majeraha ya figo (AKI), ambayo yameua […]

Categories
Uncategorized

Wakenya 31 waokolewa kutoka kwa wateka nyara huko Laos

Mnamo tarehe 31 Agosti 2022, HAART{Ufahamu Dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu}ilipokea ombi la kutaka usaidizi kupitia mitandao ya kijamii na barua pepe. Bwana mmoja aliwafahamisha HAART kwamba mwanafamilia wake ameshawishiwa kwa ahadi za uwongo za kufanya kazi Thailand ila alisafirishwa hadi Laos, pamoja na Wakenya wengine. Kwa hofu, Bwana huyo aliiomba HAART kuingilia kati […]

Categories
Education

Lamu: Hofu baada ya mimba za mapema kushika kasi

Mimba za mapema sio jambo geni nchini Kenya, ila kwa sasa, wakaazi wa maeneo ya Hindi huko Lamu wameonya hofu na wasiwasi mkuu baada ya wanafunzi sita kutoka shule ya upili ya Hindi kupachikwa mimba kwa pamoja. Kulingana na citizen, Wasichana wadogo wanapitia dhulma mbali mbali maeneo ya Hindi ikiwemo kupachikwa ujauzito wa mapema, – […]

Categories
Education Education education Latest News

Makali ya Njaa yawaweka watoto nje ya madarasa

Shuleni Kavunzoni, watoto wengi wanalilia njaa huku wengi wao wakikosa kuwa makini darasani, ni misimu minne sasa isiyo na mvua mjini Ganze kaunti ya kilifi. Udongo umemumunyuka na ardhi imekomaa, watoto hawapati chajio wala kiamsha kinywa. Imekadiria miaka mitano sasa, ambapo wenyeji hawajaweza kupanda wala kuvuna chochote kile,ila hio ndio hali ambayo watoto kama Moses […]

Categories
Education Education education

Gachagua: CBC haiendi popote

Naibu Rais Rigathi Gachagua amethibitisha kuwa Mtaala wa Kuzingatia Umahiri (CBC) hautafutiliwa mbali. Akizungumza Jumatano katika Taasisi ya Utafiti ya Cemastea, Gachagua alisema kwamba, serikali itaboresha zaidi CBC. “CBC haiendi popote, haijafutwa bali itaboreshwa tu,” alisema. Aliongoza uzinduzi wa siku tatu za kuanzishwa kwa Kikosi Kazi cha Marekebisho ya Elimu. Jopokazi la wanachama 49 liliundwa na Rais William […]

Categories
Uncategorized

Tuwalinde watoto dhidi ya ukatili

Ndani ya mwaka mmoja, takriban watoto bilioni moja wananyanyaswa kote ulimwenguni. Kila mwanadamu, bila kujali kabila, cheo, dini, elimu, au hali yoyote ile, ana haki ya kuishi katika ulimwengu wenye amani na usio na kila aina ya vurugu. Hata hivyo, kuna haja ya dharura ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi za kuzuia na kukabiliana na tishio […]

Categories
Uncategorized

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike:”Haki zetu, Mustakabali wetu”

Mnamo 2022, tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi tangu kuzaliwa kwa Siku ya Kimataifa ya Msichana (IDG). Katika miaka hii 10 iliyopita, kumekuwa na umakini mkubwa katika masuala ambayo ni muhimu kwa wasichana, haswa miongoni mwa serikali, watunga sera na umma kwa ujumla, pia kumekuwa na umuhimu chanya katika kuwapa wasichana fursa zaidi kwa kusikilizwa sauti zao katika […]