Kulingana na ripoti ya KDHS iliyotolewa leo, Kaunti ya Samburu inaongoza na asilimia 50 ya mimba za utotoni, huku Kaunti ya Nyeri na Nyandarua ikiwa na asilimia 5. Ripoti hiyo iliyofanywa na Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Nchini Kenya(KDHS), kuanzia Februari 17 hadi Julai 13, 2022, ilihusisha takriban kaya 37,911. Ripoti hiyo imeangazia […]
Author: khadija Mbesa
Watoto watatu ni miongoni mwa watu wanane waliouawa katika kijiji cha Yell Kurkum huko Laisamis, Kaunti ya Marsabit. Kulingana na polisi, washambuliaji walifyatua risasi na kuwaua wanane hao ambao kati yao kulikuwa na wanaume watano, pamoja na watoto watatu. Kamanda wa polisi wa Mashariki Rono Bunei anasema kuwa, takriban majambazi 15 waliokuwa na bunduki walivamia […]
Washirika wa afya wako tayari kutumia mkakati wa chanjo ya nyumba hadi nyumba ili kuhakikisha watoto walio katika maeneo ya mbali wanapokea dozi za surua-rubela. Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Unicef na Gavi wanaendesha kampeni ya siku 10 ya chanjo katika kaunti saba zilizo hatarini zaidi za Mandera, Wajir, Garissa, Turkana, Pokot Magharibi na […]
Zaidi ya watoto milioni 3.5 nchini Kenya wako kwenye hatari ya kukosa kuenda shule wakati zitakapofunguliwa kwa muhula wa kwanza hapo Januari mwaka ujao kwa sababu ya ukame unaoendelea, shirika la misaada ya kibinadamu la Save the Children limesema. Utafiti wa 2021 wa Global Out of School Children Initiative ulibaini kuwa kuna zaidi ya […]
Ruto Aahidi Kutokomeza Ukeketaji
Rais William Ruto amesisitiza dhamira ya serikali ya Kenya Kwanza katika kutokomeza ukeketaji hadi mwisho wa kipindi chake. Akizungumza siku ya Jumatatu, Ruto amesema kwamba, kesi za ukeketaji katika kipindi chake zitaondolewa. “Ninakubaliana na CJ Martha Koome kwamba hatufai kuwa na mazungumzo kuhusu ukeketaji nchini Kenya katika Karne ya 21,” alisema. “Ninataka kuwahakikishia uungwaji […]
Takriban wasichana 317 wajawazito ni miongoni mwa maelfu ya watahiniwa wanaofanya mtihani wa Kutathmini Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) na Cheti cha Elimu ya Msingi ya Kenya (KCPE) katika kaunti za South Rift. Jumla ya watahiniwa 292 wajawazito wanatoka katika kaunti ya Baringo, Bomet na Narok, huku wasichana 25 wajawazito wanatoka katika kaunti […]
Kulingana na baraza la DRC (Danish Refugee Council), watu Milioni 2.1 kwa sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo ya wafugaji kaskazini mwa Kenya. Viwango vya utapiamlo vinaongezeka kwa kasi, huku ikijumuisha takriban watoto 652,960 wenye umri wa miezi 6-59 na wanawake 96,480 wajawazito na wanaonyonyesha wanaohitaji matibabu ya utapiamlo uliokithiri (data ya […]
Wanafunzi wote washarudi majumbani mwao kwa likizo ndefu ambayo inakusudiwa kumalizika mwisho wa January mwaka Ujao. Hofu na wasiwasi unaongezeka juu ya utovu wa nidhamu wa watoto wakati huu wa likizo ndefu kwani mara nyingi shule huwafanya watoto kuwa na shughuli nyingi na huwaweka mbali na maovu, na hivyo kupunguza shinikizo kwa wazazi. Na hivyo, […]
Kamishna wa Kaunti ya Laikipia, Joseph Kanyiri, amesema kwamba, ombaomba hao walio na umri mdogo wanaaminika kutoka nchi jirani na wengi wao wanapatikana katika miji ya Nyahururu na Nanyuki. “Wamekuwa kichocho na hata wafanyabiashara wanalalamika kwa uwepo wao, kwani wanakaribia wanunuzi nje ya maduka makubwa wakiwa na bakuli za kuomba na wengi wao wanaendeshwa na […]
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumanne alienda karibu na eneo la vita huko Goma na Rutshuru, Kivu Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo aliwasihi wapiganaji kukomesha vita huku akikutana na watu waliokimbia makazi yao wakitoroka mapigano. Bw Kenyatta, ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nchi saba, alialikwa […]